NGUVU INAYOHITAJIKA KUWEKA MALENGO YA KUPATA MALI NA UTAJIRI NI SAWA NA ILE INAYOHITAJIKA KULETA MATESO NA UMASIKINI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NGUVU INAYOHITAJIKA KUWEKA MALENGO YA KUPATA MALI NA UTAJIRI NI SAWA NA ILE INAYOHITAJIKA KULETA MATESO NA UMASIKINI


Edson, mwanasayansi na mgunduzi mkubwa zaidi duniani, alikuwa akifanya kazi kama opereta wa simu wa muda(part time). Alifeli mara zisizohesabika kabla mwishowe hajafikishwa kwenye ugunduzi wa kipaji kilichokuwa kimelala ndani ya ubongo wake. Charles Dickens alianza kubandika lebo katika vyungu vyeusi. Mkasa wa penzi lake la kwanza ulipenya ndani ya roho yake na kumbadilisha kuwa mmoja kati ya waandishi vitabu  wakubwa kabisa wa Dunia.

Kukatishwa tamaa kunakotokana masuala ya mapenzi kwa ujumla kuna athari za kuwasukuma watu kwenye ulevi na uharibifu. Hii ni kwa sababu watu wengi hawajifunzi kamwe stadi za kugeuza hisia zao kali kuwa ndoto zenye kujenga.

Helen Keller alikuwa kiziwi, bubu, na kipofu mara tu baada ya kuzaliwa. Licha ya taabu kubwa yote iliyomkuta, jina lake limeandikwa kwa wino usiofutika katika karatasi za historia ya watu mashuhuri. Maisha yake yote yalitumika kama ushahidi kwamba kamwe mtu hashindwi, hushindwa tu pale atakapokubali kushindwa.

Robert Burns alikuwa kijana wa kijijini asiyekuwa na elimu. Alilaaniwa kwa umasikini na kukua akiwa mlevi. Dunia ilifanywa bora kwa yeye kuwa ameishi kwani alikuwa amejivika mawazo mazuri katika ushairi, hivyo kung’oa mwiba na kuotesha waridi mahala pake.

Booker T. Washington alizaliwa katika utumwa akalemazwa kwa ukabila na rangi. Kwa kuwa alikuwa mvumilivu, mwenye akili iliyofunguka muda wote, katika masuala yote, na alikuwa muotajindoto, aliacha chapa yake kwa mema katika jamii nzima.Beethoven alikuwa kiziwi, Milton alikuwa kipofu, lakini majina yao yatadumu kwa kadiri muda nao utakavyopita kwa sababu waliota ndoto na kuzibadilisha ndoto zao kuwa mawazo yaliyopangilika.

Kabla ya kuhamia kwenye sura inayofuata, amsha upya akilini mwako moto wa matumaini, imani, ujasiri na uvumilivu. Ikiwa utakuwa na hali hizi za akili, pamoja na maarifa ya kazi ya kanuni zilizoelezwa, vingine vyote utakavyohitaji vitakuja kwako utakapokuwa tayari kuvipata. Let Emerson analielezea wazo hili katika maneno yafuatayo “Kila mithali, kila kitabu, kila jambo mashuhuri lililokuwa lakwako kwa msaada na faraja kweli litakuja nyumbani  kupitia njia iliyokuwa wazi au njia iliyopindapinda. Kila rafiki, ambaye roho yako inamtamani mwishowe atakukumbatia.

Kuna tofauti kati ya kutamani kitu na kuwa tayari kukipokea. Hakuna aliyekuwa tayari kwa kitu mpaka pale atakapoamini kuwa atakipata. Hali ya akili ni lazima iwe na imani na siyo matumaini matupu ama matamanio. Utayari wa akili ni muhimu kwa imani. Akili iliyofungwa haihamasishi imani, ujasiri wala kuamini.

Kumbuka, nguvu inayohitajika kuweka malengo makubwa maishani katika kupata mali na utajiri ni sawasawa na ile inayohitajika kuleta mateso na umasikini. Mshairi mashuhuri kwa usahihi kabisa ameeleza ukweli huu  unaokubalika na kila mtu kupitia mistari ifuatayo;
Nilijadiliana bei na maisha,
Na maisha hayakutaka kuongeza pesa zaidi.
Hata hivyo niliomba tena jioni,
Nlipokuwa nafunga hesabu za duka langu dogo

Kwa kuwa maisha ni mwajiri tu,
Hukupa tu kile unachokiomba.
Lakini mara unapokuwa umepanga mshahara,
Kwanini, ni lazima utimize wajibu

Nilifanya kazi ya hali ya chini,
Kujifunza tu, mvunjiko wa moyo,
Kwamba mshahara wowote niliokuwa nimeomba,
Maisha yangelikuwa tayari kulipa.

Shauku Hushinda Asili
Kama kilele muafaka cha sura hii, natamani kumtambulisha mmoja kati ya watu wasiokuwa wa kawaida zaidi niliopata kuwajua. Nilimuona kwa mara yangu ya kwanza dakika chache baada ya kuzaliwa. Alikuja duniani pasipokuwa na dalili zozote za masikio ya kawaida na daktari alikiri  hilo alipoulizwa atoe maoni yake kuhusu kama mtoto angeweza kuwa kiziwi na bubu kwa maisha yake yote.

Niliyapinga maoni ya daktari. Nilikuwa na haki ya kufanya hivyo; nilikuwa baba wa mtoto. Na mimi pia nilifikia uamuzi na kutoa pendekezo, lakini nililisema pendekezo hilo kimya kimya, sirini ndani ya moyo wangu. Niliamua kwamba kijana wangu angeweza kusikia na kusema.

Asili ingeweza kunitumia mtoto asiyekuwa na masikio, lakini asili isingeweza kunishawishi kukubali ukweli wa mateso. Ndani ya akili yangu nilijua kwamba kijana wangu angeweza kusikia na kusema. Kwa jinsi gani? Nilikuwa na uhakika ni lazima kuna njia, na hili nilifahamu ningeweza kuipata. Niliyafikiria maneno ya Bwana Emerson yasiyokufa “ Mlolongo mzima wa mambo unaenda kutufunza imani. Tunahitaji tu kutii. Kuna mwongozo kwa kila mmoja wetu, na kwa kusikiliza kwa unyenyekevu, tutaweza kusikia neno sahihi”


Neno sahihi? SHAUKU! Zaidi ya kitu kingine chochote, Nilikuwa na shauku kwamba kijana wangu asiwe kiziwi bubu. Kutoka shauku hiyo sikurudi nyuma hata sekunde moja. Miaka mingi kabla niliandika hivi; “Mipaka yetu pekee ni ile tunayojiwekea ndani ya akili zetu”. Kwa mara ya kwanza, nilishangaa ikiwa usemi huo ulikuwa kweli. 

Akiwa amelala kitandani mbele yangu alikuwa mtoto mchanga aliyezaliwa, pasipokuwa na vyombo vya asili vya kusikia. Hata kama angeliweza kusikia na kusema, alikuwa dhahiri mwenye ulemavu maisha yake yote. Ukweli, hiki kilikuwa kikwazo ambacho mtoto yule hakuwa amejiwekea katika akili yake mwenyewe. Ni kitu gani ambacho ningeliweza kufanya juu ya hilo?








0 Response to "NGUVU INAYOHITAJIKA KUWEKA MALENGO YA KUPATA MALI NA UTAJIRI NI SAWA NA ILE INAYOHITAJIKA KULETA MATESO NA UMASIKINI"

Post a Comment