MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA KISINGIZIO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA KISINGIZIO


Na wewe pia waweza kujua kwamba kila kiongozi mkubwa  tangu mwanzo wa ustaarabu mpaka sasa hivi alianza na ndoto. Ikiwa hautaweza kuuona utajiri mkubwa katika fikra zako, basi kamwe hautaweza kuuona katika balansi yako ya benki. Kamwe haijawahi kuwepo fursa kubwa kwa waotajindoto kivitendo kama ilivyokuwa sasa.

Sisi ambao tulio katika mbio za kusaka utajiri tunapaswa kutiwa moyo kufahamu kwamba, Dunia hii inayobadilika, ambamo tunaishi ndani yake, inahitaji mawazo mapya, njia mpya za kutenda mambo, viongozi wapya, ugunduzi mpya, njia mpya za kufundisha, njia mpya za kutafuta masoko, vitabu vipya, fasihi mpya, matumizi mapya ya kompyuta, tiba mpya za maradhi na njia mpya kwa kila nyanja ya biashara na maisha.

Nyuma ya mahitaji hayo kwa vitu vipya na vizuri zaidi kuna sifa moja ambayo mtu ni lazima kwanza awe nayo kusudi aweze kushinda, nayo ni, ukamilifu wa lengo, elimu ya ni nini mtu anachokitaka, pamoja na shauku kuu ya kukimiliki.

Ili kutimiza hilo, anatakiwa muotajindoto kivitendo ambaye anaweza, na atakayeziweka ndoto zake katika vitendo. Waotajindoto kivitendo daima wamekuwa, na daima watakuwa wachora kielelezo cha ustaarabu. Sisi tuliokuwa na shauku ya kujichumia utajiri, tunapaswa kukumbuka kwamba viongozi wa kweli wa Dunia, daima wamekuwa watu wenye kutumia, na kuweka katika vitendo nguvu isiyoshikika wala kuonekana ya fursa ambayo bado haijazaliwa. Wamebadilisha nguvu hizo (au msukumo wa fikra) kuwa majengo marefu, miji mikubwa, viwanda, ndege, magari, huduma bora za afya na kila aina ya hali bora inayofanya maisha kuwa yenye furaha.

Ustahimilifu na akili iliyofunguka ni mahitaji ya kivitendo kwa muotajindoto wa leo. Wale ambao ni waoga wa mawazo mapya hushindwa kabla hawajaanza. Haijawahi kutokea wakati muafaka zaidi kwa waasisi  kushinda sasa. Kuna biashara nyingi zisizomithilika, dunia ya kifedha na kiviwanda kuumbwa tena upya na kuelekezwa sambamba na njia mpya zilizokuwa bora zaidi.

Katika kupanga kupata mgawo wako wa utajiri, usiruhusu mtu akushawishi kumdharau muotajindoto. Kuvishinda vigingi vikubwa katika hii dunia inayobadilika kila wakati, ni lazima uwe na roho ya waasisi wakubwa wa zamani ambao ndoto zao zimeupa ustaarabu kila kitu cha thamani uliyokuwa nacho, roho ambayo hutumikia mithili ya damu ya uhai wa jamii yetu-nafasi yako na yakwangu, kuendeleza na kutafuta soko la vipaji vyetu.


Tusisahau, Columbus aliota juu ya Dunia isiyojulikana, akihatarisha maisha yake kwa uwepo wa dunia hiyo, na aliivumbua! Copernicus, mwana-elimu ya anga, aliota juu ya uwepo wa sayari nyingi, na hilo alilithibitisha! Baada ya kusherekea ushindi hakuna mtu aliyemshutumu hadharani kuwa aliyoyasema yalikuwa hayatekelezeki. Badala yake Dunia ilitoa heshima kubwa kwenye kaburi lake, hivyo kuthibitisha kwa mara nyingine tena kwamba, mafanikio hayahitaji kuomba radhi, kushindwa hakuna kisingizio.

Itaendelea sehemu ya nne...........

------------------------------------------------------------------------------------

0 Response to "MAFANIKIO HAYAHITAJI KUOMBA RADHI, KUSHINDWA HAKUNA KISINGIZIO"

Post a Comment