Kitabu cha Think and Grow Rich(Fikiri Utajirike) au ‘Msahafuwa mafanikio’ kama kilivyobatizwa na Self Help Books Tanzania Limited, kilianza
kutafsiriwa katika lugha ya kiswahili kwa mara ya kwanza kabisa na kampuni hiyo
hapo mwaka 2012 kwenye tovuti na blogu yake iliyokuwa ikijulikana kama “KUELEKEAUTAJIRI”
na baadaye kuja kuitwa, “JIFUNZEUJASIRIAMALI”.
Lengo letu ni kuhakikisha wapenzi wa kitabu hiki maarufu
zaidi duniani na kilichowahi kuuzwa nakala nyingi kuliko kitabu kingine
chochote katika tasnia hii, wanaweza wakakisoma katika lugha yao ya mama yaani
kiswahili fasaha bila ya bughudha zozote za kuwa na kamusi pembeni, “English-swahili
dictionary”, kila mara wanapotaka kukisoma.
Bado kazi ya kuendelea kukichapisha kitabu hiki kidogokidogo
katika lugha ya kiswahili inaendelea kwenye blogu ya jifunzeujasiriamali ambapo
hadi kufikia sasa tumefika sura ya 4. Pamoja na kukichapisha huko kizima kama
kilivyo, pia tumeona ipo haja ya kuweka muhtasari mzima wa kitabu hicho sanjari
na mfululizo huo kusudi wasomaji watakaopenda kukisoma kitabu hicho cha Think
and Grow Rich kwa ufupi nao waweze kufanya hivyo bila shida.
Hata hivyo muhtasari au ufupisho wa kitabu, kamwe hauwezi
ukawa mbadala wa kitabu chenyewe, utamu na maana halisi ya kitabu unaweza
ukavipata kwa kusoma kitabu chote na wala siyo ufupisho wake. Kuna “details
nyingi” vitu vya ndani ambavyo hauwezi kabisa ukavijumuisha katika uchambuzi wa
kitabu na ili uweze kuvipata vitu hivyo kwa ubora wake halisi ni lazima usome
kitabu kama kitabu kikiwa kizima.
Hata hivyo, Uchambuzi wa vitabu, mapitio au kitabu kwa
ufupi vina faida zake nyingi ikiwa ni pamoja na kumrahisishia msomaji kupata
picha ya kitabu kizima katika muda mchache, kupata maudhui ya vitabu vingi
katika muda mfupi pamoja na kukwepa kusoma baadhi ya vitu ambavyo havina
umuhimu mkubwa kwake.
Lakini kuna vitabu ambavyo hata kama utasoma ufupisho
wake lakini baadaye utahitaji pia kukisoma kitabu kizima. Vitabu vya namna hiyo
ni vile vitabu ambavyo kamwe hautaweza kuvisahau maishani mwako. Kitabu
kama hiki ‘Think and Grow Rich’, kitabu kilichowahi kusomwa na
karibu watu wote unaowajua wenye mafanikio duniani, wakiwemo kina Barack Obama,
Bill Gates, Ophrah Winfrey, Nelson Mandela, Muhammad Ali, John F.Kennedy, Reginald
Mengi, Mohamed Dewji, Eric Shigongo na wengineo wengi, sidhani kama ungependa ukisome kwa ufupi tu na
kisha uachie hapo hapo, ni lazima upange kuja kukisoma chote kizima na hii ndiyo
sababu iliyotusukuma sisi SHBPL kukitafsiri kitabu hicho kusudi wasomaji waweze
kukisoma kwenye blogu yao ya jifunzeujasiriamali.
Mapitio hayo kwa ufupi tutakuwa tukiyafanya pia kwa
vitabu vingine mbalimbali vya elimu ya pesa na mafanikio(vile muhimu zaidi).
kumbuka duniani kuna maelfu ya vitabu vya aina hiyo na wala hata useme kwa
mfano mtu unataka usome kila kitabu cha mafanikio duniani, utazeeka ungali bado haujafikisha hata robo yake. Kikubwa na
cha msingi ni mtu kuchagua vitabu vyako vya maana ukaamua hivi nitavisoma
kikamilifu na kufanyia kazi barabara yale utakayojifunza. Hautaishia hapo
kusoma kwani kazi ya kusoma haina mwisho mpaka unaingia kaburini lakini huwezi
ukaniambia utasoma bila ratiba na ikiwa utatumia ratiba basi ni lazima
tukubaliane ile kanuni ya msingi ya asili isemayo, “Kupanga ni kuchagua, hatuwezi
duniani tukafanya kila kitu kilichopo mbele yetu, muda mara zote huwa kikwazo” .
Ukipenda kufahamu zaidi juu ya falsafa yangu hiyo,
nakushauri udownload hapa bure kitabu nilichotunga kiitwacho, Kanui ya kujifunza Elimu ya Pesa naMafanikio kwa Ufanisi mkubwa”. Nimeipa jina kanuni hiyo kuwa (Peter’s Theory of studying Success Books).
Wahi mapema kwani kitabu hicho kizuri hivi karibuni kitaingia katika Orodha ya
vitabu vinavyouzwa na bei yake itakuwa ni Tsh. 5,000/=.
Kuanza kusoma mapitio au uchambuzi wa kitabu Think and
Grow Rich kwa lugha ya kiswahili fasaha, bonyeza maandishi yafuatayo hapo chini;
0 Response to "THINK AND GROW RICH KWA UFUPI: MAPITIO YA VITABU VYA MAFANIKIO(BOOKS-REVIEW)"
Post a Comment