MUHTASARI WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA PILI 2 (UCHAMBUZI YAKINIFU) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MUHTASARI WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA PILI 2 (UCHAMBUZI YAKINIFU)

SURA  YA  2.
(MWANZO WA MAFANIKIO YOTE.)
Hatua ya kwanza kuelekea  utajiri.
Kuwa na shauku (hamu kubwa ya kupata mafanikio)
Edwin C. Barnes alipopanda treni kwenda kumfuata mvumbuzi mashuhuri  Bwana Thomas Edison, ungeweza kumfananisha na omba omba au mzururaji asiye na kazi ya kufanya, lakini  ndani ya akili yake alibeba wazo lenye thamani ya mamilioni ya dola. Yeye mwenyewe kabla hajafika kwa  Edison akilini alijijengea picha kama kwamba tayari ameshakuwa mbia, ingawa bado hata hakuwa ameonana naye. Alipofika  aliomba kibarua kama mtumishi wa ndani.Miaka  mitano baadaye ndoto yake ikaja kugeuka kuwa  kweli.

Ili kugeuza hamu au shauku yako kubwa kuwa kitu halisi yapo mambo sita unayopaswa kuyafanya;
1)  Tengeneza picha akilini mwako ya kiasi hasa cha kile kitu unachotaka, kama ni fedha jiwekee kiasi kamili kwa mfano "nataka niwe na Shilingi milioni 50."
2)  Fahamu kwa uhakika ni ni kipi utakachotoa ili kufanikiwa.
3)  Panga au weka tarehe/muda maalumu utakapofanikisha jambo hilo.
4)  Tengeneza mpango mahsusi wa kuigeuza hiyo ndoto yako na uanze mara moja pasipo kujali kama upo tayari au bado.
5)  Andika katika karatasi kile kitu ulichopanga kukipata mathalani kiasi cha fedha, muda utakaochukua pamoja na kile utakachokitoa kama malipo.
6)  Soma kile ulichoandika kwa sauti kila siku mara mbili, asubuhi mara unapoamka na usiku kabla haujaenda kulala.Wakati unapokuwa ukisoma jione na kujihisi mwenyewe kama vile tayari unakimiliki kile ulichokiwekea malengo.Hakuna mtu yeyote awezaye kumiliki kitu pasipo kwanza kuamini kuwa anao uwezo wa kukimiliki.


>>>Kufunguasura inayofuata>>>>             
  

<<<Kurudisura iliyopita<<<<<<<<<                               

0 Response to "MUHTASARI WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA PILI 2 (UCHAMBUZI YAKINIFU)"

Post a Comment