LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO


Kwa upendo jaribu kumpa taarifa ya ua hili  jirani, rafiki na ndugu zako ili wawe makini kwa ua hili. Basi ngoja mimi Kapulya niwatakieni siku njema  na tutaonana tena panapo majaliwa. Jumatano njema!!

Ujumbe huu nimeuona katika blogu ya Maisha na mafanikio na kwa kuwa mwenye blogu ameruhusu ujumbe usambazwe kwa jirani nami nikaamua niitikie wito kwa kuuweka moja kwa moja hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali kwani ni jambo jema kuwalinda hasa watoto wetu na vitu vinavyoweza kuhatarisha maisha na afya zao.

Binafsi nimeshtushwa sana na ua hili, sijui kama nalifananisha au ni vipi kwani kipindi nikiwa mdogo kijijini nilikuwa nikiona ua linalofanana na hilo na lilikuwa likipandwa katika bustani ya maua na mama zangu wadogo, sijui ikiwa walikuwa wanafahamu kama lilikuwa hatari kiasi hicho au la. Nitajaribu kufanya utafiti zaidi kuulizia ikiwa ndilo na kama watu wanafahamu hatari yake.

0 Response to "LINAONEKANA NI UA ZURI LAKINI NI HATARI SANA LINAWEZA KUUA MTOTO CHINI YA DAKIKA KUMI NA TANO"

Post a Comment