Nimepokea simu na barua pepe
za wasomaji wetu wengi wakitaka tuweke historia za watu mashuhuri hasa
matajiri, wanamuziki, wacheza filamu, wacheza soka na wengineo, lakini tujikite
zaidi katika utajiri waliokuwa nao na jinsi walivyoweza kufanikiwa, ni mbinu
zipi walizozitumia mpaka wakapata mafanikio hayo.
Bila shaka kila mtu
anayefanikiwa maisha ni lazima awe mjasiriamali, kwa hiyo basi katika makala
tutakazokuwa tukizijadili kuhusiana na mada hiyo kwenye blogu hii tutajaribu
kuwachambua watu hao maarufu kusudi tuweze kubaini ni tabia gani, au sifa zipi
za kijasiriamali zilizoweza kuwafikisha pale walipo. Kumbuka tabia/sifa za
kijasiriamali zipo nyingi lakini inategemea ni ipi na katika mazingira gani mtu
ameitumia.
Miongoni mwa wasomaji waliotuma
ushauri ni pamoja na Mbaruk wa Bukoba, yeye ameshauri ikiwezekana tuwe
tunasimulia jinsi watu mbalimbali mashuhuri na matajiri walivyoweza kufikia
pale walipo na sababu zilizowanyanyua. Anselm Sabas wa Moshi yeye aliomba
nyimbo mbili za mwanamuziki mashuhuri Afrika Mashariki Jose Chameleon, Tubonge
na Valuvalu, tafsiri ya mashairi yake, utajiri aliokuwa nao pamoja na historia
yake kimaisha kwa ujumla.
Tunathamini mno maoni na ushauri wa wasomaji wetu, hivyo
kuanzia leo tutaanza kutekeleza kile mlichoomba bila ya hiyana na kwa kuanza
basi tumeonelea tuanze na huyu Gwiji Jose Chameleon kutoka nchini Uganda na
kabla ya yote kwanza hebu tuzisikilize ngoma zake mbili pamoja na video
zilizoombwa na msomaji wetu kutoka moshi Anselm Sabas.
Tubonge wimbo uliompa chameleone umaarufu mkubwa.
Video ya wimbo huo Tubonge(official video)
Sasa unaweza kudownload mp3 ya wimbo wa Valu valu hapa.
VIDEO ya wimbo Valu valu,tazama hapa chini.
0 Response to "NAOMBA NYIMBO ZA JOSE CHAMELEONE: TUBONGE NA VALU VALU"
Post a Comment