NI AKINA NANI WANAOHITAJI MPANGO/MCHANGANUO WA BIASHARA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI AKINA NANI WANAOHITAJI MPANGO/MCHANGANUO WA BIASHARA?



Mchanganuo wabiashara au mpango wa biashara unahitajika na watu mbalimbali ukiwemo wewe mwenyewe mmiliki wa biashara na umuhimu wake kwako wewe mwenyewe biashara tofauti na inavyodhaniwa na watu wengi, ni mkubwa zaidi hata kushinda wadau wengine kama benki taasisi za fedha na wabia. Hebu tutazame sasa ni watu gani wanaohitaji mpango wa biashara,

1)  Wale wanaotaka kuanzisha biashara mpya ni lazima wawe na mipango ya biashara ili kufahamu kwa uhakika ikiwa biashara zao zitalipa pamoja na kusaidia kuwaonyesha njia ni kitu gani wanapaswa kufanya ili wafanikiwe. Kama unafanya biashara pasipo kuwa na mpango wa biashara ni sawa na mtu anayetembea njiani angali amefumba macho.


2)  Wenye biashara zilizokwisha anzishwa siku nyingi nao wahahitaji mipango ya biashara ili kuzipanua na kuziboresha zaidi pamoja na kuitumia katika kuomba mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha.Utakuwezesha kufahamu pale ulipo, ulikotoka na unakotaka kwenda.



3)  Wawekezaji, mameneja wa mabenki na wabia huhitaji kuona michanganuo ya biashara inayogusa maeneo yote yanayoihusu biashara ili wajiridhishe kuwa ni kweli mjasiriamali amejizatiti na yuko makini na kitu anachotaka kukifanya.




4)  Ikiwa wewe ni mfanyakazi katika taasisi fulani ni lazima bosi ama mabosi wako wahitaji mchanganuo kamili wa biashara kwa miradi itakayoanzishwa na taasisi kwa ajili ya utekelezaji.

5)  Wanafunzi katika taasisi mbalimbali za elimu kama vyuo vikuu na vituo vya kuendeleza biashara ndogondogo pamoja na wahadhiri wao au wakufunzi huhitaji michanganuo ya biashara katika kujifunza ujasiriamali na namna ya kuiandika michanganuo yenyewe.


0 Response to "NI AKINA NANI WANAOHITAJI MPANGO/MCHANGANUO WA BIASHARA?"

Post a Comment