KWANINI TULIBADILISHA JINA “KUELEKEAUTAJIRI” KUWA JIFUNZEUJASIRIAMALI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI TULIBADILISHA JINA “KUELEKEAUTAJIRI” KUWA JIFUNZEUJASIRIAMALI?

Awali kitabu kikubwa chenye kurasa 410 kilichosheheni karibu kozi/mada  zote za ujasiriamali na biashara pamoja na michanganuo ya biashara halisi iliyokamilika ipatayo 50 tulikiita “KUELEKEAUTAJIRI”. Vilevile Tovuti na Blogu tulizipa jina hilohilo.

SABABU ZA KUTUMIA JINA HILO.
Kwa kuwa Lengo letu kuu ni kutokomeza umasikini, tuliamua kulitumia jina hilo kama kaulimbiu(slogan) yetu ya kuwahamasisha wasomaji kusudi waweze kujifunza mbinu mbalimbali za ujasiriamali na biashara. 

Na chanzo hasa cha jina hili ni kutoka katika kitabu maarufu zaidi Duniani cha Mafanikio  kuwahi kuandikwa, THINK & GROW RICH” Nadhani ni kutokana na watendaji katika kampuni yetu kuathiriwa mno na falsafa za kitabu hiki ndiyo maana tukajikuta tukilitumia neno hilo pasipokupima athari ambazo zingeliweza kutokea kwa wasomaji.

Mwandishi wa kitabu hicho Napoleon Hill katika kila sura za kitabu chake kuanzia sura ya pili alizibatiza kila moja kuwa ni “HATUA KUELEKEAUTAJIRI”. Kwa mfano Sura ya pili ameiita ni ‘Hatua ya kwanza kuelekeautajiri’, kwa kimombo “The firs step toward riches ushahidi kutoka katika kitabu hicho ni huu hapa chini,



SASA KWANINI TULIBADILISHA JINA HILI?
1. UTATA: Baadhi ya wasomaji wetu hasa wale wa kwenye Tovuti na Blogu hawakutuelewa, wengi walidhania kwamba “KUELEKEAUTAJIRI”  ni miongoni mwa Taasisi au  Vyama vyenye utata kwenye jamii, vinavyohusishwa na kuwapatia watu Utajiri kwa njia za kimiujiza au kwa siri. Tuligundua hilo baada ya kupokea simu za watu wengi waliokuwa wakiuliza kama tunaweza kuwaunganisha na vyama au taasisi za namna hiyo. Jibu letu kwao kila mara lilikuwa ni “HAPANA, WALA HATUNA UHUSIANO WOWOTE NA TAASISI ZA NAMNA HIYO”

Lakini ili kuiondoa dhana hiyo tata, tulifanya uamuzi wa kubadilisha jina hilo na sasa, Kitabu chetu kikubwa kinaitwa JIFUNZE MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” huku Tovuti na Blogu zikiitwa, jifunzeujasiriamali.com na jifunzeujasiriamali.blogspot.com

Utakapokutana na neno/jina ‘Kuelekeautajiri’ katika vitabu vyetu mbaliimbali, ni kwa sababu vilichapishwa muda kabla ya mabadiliko haya kufanyika. Ikumbukwe mabadiliko hayajagusa maudhui/yaliyomo ndani ya vitabu hivyo wala tovuti , blogu na mitandao mingine ya kijamii.

Dhamira yetu kuu sisi ‘SHBPL’ ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuendesha biashara zao kwa ufanisi wa hali ya juu, na wala siyo vinginevyo.

Ahsanteni, Tunawatakia usomaji mwema.



0 Response to "KWANINI TULIBADILISHA JINA “KUELEKEAUTAJIRI” KUWA JIFUNZEUJASIRIAMALI?"

Post a Comment