KING KESTER EMENEYA, VICTORIA ELEYSON MBUYU MWINGINE TENA ULIODONDOKA KONGO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KING KESTER EMENEYA, VICTORIA ELEYSON MBUYU MWINGINE TENA ULIODONDOKA KONGO

King Kester 
Tabu Ley Rochereau’s kabla  hata hajakaa kaburini miezi 2, kinasikika tena kishindo kingine kikuu cha kuanguka kwa ‘mbuyu’ mwingine, gwiji la muziki wa Kongo King Kester Emeneya. Emeneya pamoja Wanamuziki   kama kina Papa wemba, Kofi Olomide, Felix Wazekwa, Dindo Yogo na wengineo kibao nikiwataja hapa nitakesha, waliutikisa Ulimwengu wa muziki wa Kikongo vilivyo miaka hasa ya 80, 90 na hata sasa katika Bara la Afrika hususana Afrika ya kati na Mashariki.
 
Marehemu King Kester Emeneya

Kasha la kanda ya Album lilikua  hili

Nakumbuka vizuri sana kipindi kile nasoma, miaka ya 90, tulivyokuwa tukikatika mayenu na wimbo huu wa Victoria Elyson Dandy siwezi kuusahau kamwe, kwani  siku moja katika sherehe ya ubarikio, tulifanya show ya kufa mtu huku watu wakitutuza utadhani tulikuwa tunatoka Kongo vile.


0 Response to "KING KESTER EMENEYA, VICTORIA ELEYSON MBUYU MWINGINE TENA ULIODONDOKA KONGO"

Post a Comment