TWENDE NAIROBI WA TABU LEY NA MBILIA BEL WIMBO ULIOBADILISHA HARAKA MSIMAMO WA RAIS MOI KENYA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TWENDE NAIROBI WA TABU LEY NA MBILIA BEL WIMBO ULIOBADILISHA HARAKA MSIMAMO WA RAIS MOI KENYA

Tabu Ley na Mbilia Bel
Miaka ya 80 Kenya ilipokuwa na stesheni moja tu ya redio ‘Sauti ya Kenya’ iliyokuwa ikimilikiwa na Serikali, iliamua kuzipiga marufuku nyimbo zote za nje kuchezwa katika redio hiyo.

Haraka, Tabu Ley Rochereau alitunga kibao kikali na kitamu cha muziki kilichojulikana kama ‘Twende Nairobi’ na ambacho kiliimbwa na aliyekuwa mkewe Mrembo Mbilia Bel. Kibao hiki kizuri kilimsifia rais Moi na mara moja kikaupoza moyo wa rais na akabatilisha mara moja marufuku iliyokuwa imewekwa.


Kubadilisha  msimamo wa Rais hasa nyakati zile za chama kimoja haikuwa jambo rahisi, lakini kwa wanamuziki wa Kongo (Zaire) wa kipindi kile walikuwa na uwezo huo, kwani hata Marehemu Luambo Luanzo Makiad naye inasemekana kuna wakati aliuteka sana moyo wa aliyekuwa Dikteta wa nchi hiyo Marehemu Mobuttu Seseseko.

Tabu Ley Rochereau enzi za uhai wake akiwa na mpenzi wake Mbilia bel
Tabu ley jana alifariki  Dunia akiwa katika hospitali moja nchini Ubelgiji alikokuwa amelazwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na kiharusi kilichompata mwaka 2008. 

Atakumbukwa kwa nyimbo zake kali zaidi ya 2000 ukiwemo uliompatia chati ya juu sana, MUZINA pamoja na album zipatazo 250, huku akiwa ameibua vipaji kibao vya wanamuziki wengine akiwemno aliyewahi kuwa mke wake Mwanadada mrembo Mbilia Bel


Hebu sikiliza audio ya wimbo hapa na kuona video ya kibao hicho,Twende Nairobi, Nakei Nairobi;

Audio, wimbo wa Twende Nairobi uliomfanya Rais Moi wa Kenya anywee ghafla



VIDEO YA TWENDE NAIROBI.

0 Response to "TWENDE NAIROBI WA TABU LEY NA MBILIA BEL WIMBO ULIOBADILISHA HARAKA MSIMAMO WA RAIS MOI KENYA"

Post a Comment