SAFARI YA INDIA KWENDA SAYARI YA MARS YAKWAA KISIKI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SAFARI YA INDIA KWENDA SAYARI YA MARS YAKWAA KISIKI

Kile chombo kilichorushwa na Idara ya mambo ya Anga za juu ya India hivi karibuni kwenda Sayari nyekundu ya Mars  kimekwaa kisiki baada ya injini yake kufeli kukirusha chombo hicho kutoka katika tabaka la nguvu za uvutano la dunia.

Tatizo hilo lilitokea marekebisho yalipokuwa yakifanywa ili kukiongezea nguvu ili kiweze kufikia kasi yake ya juu kutoka Km.71,623 hadi Km.100,000 ili kuweza kufikia umbali wake wa juu. Hata hivyo Mkuu wa shirika la utafiti wa anga alisema chombo hicho bado kingali dhabiti.

Kutokana na tatizo hilo, chombo hicho sasa hakitaruka tena moja kwa moja kuelekea Sayari ya Mars na badala yake itabidi kiendelee kuizunguka Dunia mpaka pale matengenezo muhimu yatakapofanywa ili kiwe na uwezo wa kulivuka tabaka la nguvu za uvutano la Dunia kuelekea anga za juu zaidi zilipo sayari nyinginezo ikiwemo na hii ya Mars.


Ikiwa nchi ya India itafaulu katika jaribio lake hili, itakuwa ni Taifa la nne baada ya Marekani, Urusi na Jumuiya ya Ulaya kurusha chombo kwenda katika Sayari hii ya Mars. 

0 Response to "SAFARI YA INDIA KWENDA SAYARI YA MARS YAKWAA KISIKI"

Post a Comment