MAISHA SAYARI MPYA YAJA, JIANDAE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAISHA SAYARI MPYA YAJA, JIANDAE

Sayari ya Mars
Licha  ya Wanasayansi  kutoka mataifa makubwa yakiwemo Marekani ,Urusi na Uingereza mpaka sasa hivi kutokupata uwezekano wa Sayari ya Mars kufaa kuishi binadamu, bado harakati na tafiti zinaendelea  na makundi mbalimbali kutafuta uwezekano wa binadamu kuishi katika Sayari hii nyekundu.

Hivi karibuni mwaka 2011 iliibuka Taasisi moja isiyokuwa ya kiserikali inayojiita MARS ONE na kudai kwamba ina malengo ya kuhakikisha mpaka ifikapo mwaka  2022  iwe imeshapeleka watu wane kuishi katika sayari ya Mars na itaendelea na kupeleka wengine kidogokidogo.


Ikumbukwe kwamba Baada ya mashindano ya  Wamarekani na Warusi miaka ya 60 na 70 kupeleka vyombo mbalimbali na watu katika anga za juu Marekani hatimae  walifanikiwa  kuwa wa kwanza kupeleka chombo katika sayari ya Mars lakini kisichokuwa na binadamu ndani mnamo June 19 mwaka 1976, chombo hicho Viking 1 kilikuta uwezekano wa binadamu kuishi pale haupo kabisa kutokana na hali ya hewa kuwa baridi mno na hamna maji.  

Wamarekani hao hao tena wakawa wakwanza kupeleka binadamu wa kwanza akatua katika  uso wa mwezi mnamo July 20 1969 wakiwa na chombo kilichoitwa Apollo 11.

Sputnic satelite ya kwanza angani
Kwa upande wa Warusi wao wanasifika sana kwamba ndio wa kwanza kabisa kurusha setilaiti ya kwanza angani na kuizunguka Dunia ‘Sputnic’ wakati huo iliwafanya Wamarekani kuduwaa na kuigwaya Urusi kiasi kwamba Wamarekani ndipo walipoanzisha rasmi mashindano ya kutuma vyombo angani. Ilikuwa ni mwaka  1957 mwezi Octoba tarehe 4.

Mpaka sasa hivi  Shirika la NASA lA Marekani na hata nchi nyinginezo kama Uchina, wanaendelea na misheni mbalimbali  anga za juu kutafuta uwezekano wa binadamu kwenda kuishi huko, au hata kujua kama kuna viumbe wenye uhai wanaoishi katika sayari nyingine tofauti na dunia hii lakini hamna dalili yeyote zaidi ya Mars kuonekana kama iliwahi kuwa na maji miaka mingi iliyopita lakini haijabainika bado yalikokwenda ni wapi.

Viking 1 chombo cha kwanza kutua Mars
Sayari ya Mars ardhi yake ni nyekundu sana kutokana na madini ya chuma, ina baridi kali mno kufikia nyuzi joto (-107) sawa na -161F , Presha yake iko chini sana 600pa na anga limejaa hewa ya ukaa (CO2). Ipo pia miale hatari  ya jua ijulikanayo kama ‘Solar wind’ na ‘Cosmic radiation’  vitu vinavyoifanya iwe hatari zaidi binadamu yeyote kuishi huko.

Hali hii inafanya uwezekano wa Binadamu kwenda kuishi Sayari ya Mars  kuwa mdogo sana na hata hii taasisi ya Mars One huenda ina agenda zake nyinginezo kama vile kujikusanyia fedha kiujanja na siyo kuwapeleka watu wakaishi Sayari ya Mars kama inavyodai.

Lakini pia hatuwezi tukapinga kabisa uwezekano huo kwani ikiwa vitatengenezwa vyombo maalumu mfano wa Apollo na ambavyo vitawekewa mazingira ndanio yake yanayofanana na humu duniani basi jambo hilo litawezekana. Hata hivyo kitu kama hicho ni gharama kubwa sana, na pengine hata yachange Mataifa makubwa mawili au matatu haitakuwa rahisi hata kumuweka binadamu mmoja pale kwa masaa, sembuse kwenda kushika kiwanja kule cha kulima.


Madai kwamba viongozi mbalimbali wakiwemo Maraisi wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza kumiliki viwanja huko nayo ni kutia chumvi tu kunakofanywa na taasisi hiyo kusudi “Wajinga” wajiunge na kupeleka pesa zao kwao mithili ya ‘DESI’ 

Chanzo, mitandao mbali mbali ikiwemo, WIKIPEDIA, na  MARS ONE 

0 Response to "MAISHA SAYARI MPYA YAJA, JIANDAE"

Post a Comment