JEFRYDER NA NGOMA NIPE LOVE, NIPE MIC, MJASIRIAMALI WA HIP HOP ANAYEKUJA KWA KASI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JEFRYDER NA NGOMA NIPE LOVE, NIPE MIC, MJASIRIAMALI WA HIP HOP ANAYEKUJA KWA KASI

Tuko majirani katika shughuli zetu za kila siku, lakini mpaka nakuja kujua kwamba kijana huyu ni msanii mwimbaji wa Bongo fleva au tuseme hip hop kama yeye mwenyewe anavyo sema ni baada ya kumuuliza juu ya wimbo mmoja ambao nilikuwa nikiusikia ukipigwa sana redioni, ‘Nipe love’ kwamba ni nani aliyeupiga.

Jefryder akifanya shooting ya wimbo wake 'Nipe mic'  
Kwa hakika wimbo huu mimi binafsi naupenda mno, na nilishangaa sana aliponiambia kwamba ni wimbo wake. Jafary Ahmed au kwa jina la usanii ‘JEFRYDER’ ni kijana aliyeamua kujiajiri mwenyewe kupitia sanaa ya muziki wa kizazi kipya hususan Hip Hop. Mpaka sasa hivi ameshatoa ngoma kali mbili, hii ya Nipe love na nyingine ambayo amenieleza ni jana tu amemalizia kufanya video yake inayokwenda kwa jina la NIPE MIC. Anasema  “ Inshaalah Kwa Rehma za Mwenyezi Mungu, Muumba wa vyote, video hiyo inaweza ikaanza kurushwa hewani  mwanzoni mwa mwezi Oktoba”

Jefryder katika shooting ya Nipe mic
Kijana Jefryder anachoomba kwa wadau wote wa muziki ni ‘support,’ anasema angefurahi sana endapo atapata watu wa kumfadhili ili aweze kutimiza malengo yake katika muziki ikiwa ni pamoja na gharama mbalimbali za kurekodi pamoja na kufanya shooting za video za nyimbo zake. Anasema anazo track nyingi ambazo tayari ameshaziandaa lakini kikwazo ni gharama. Ikiwa atapata sapoti ya kutosha anasema atatoa album itakayomtambulisha vizuri zaidi.

Jeff akiendelea kuchana mistari
Hapa chini ni ngoma zake mbili Nipe Love na ya pili ni Nipe Mic, zisikilize ni nzuri kwa kweli.


0 Response to "JEFRYDER NA NGOMA NIPE LOVE, NIPE MIC, MJASIRIAMALI WA HIP HOP ANAYEKUJA KWA KASI"

Post a Comment